Muwekezaji wa klabu Bingwa Tanzania Bara Mohamed Dewji Mo, amekasimu madaraka ya uenyekiti kwa aliyekua makamu mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya klabu hiyo Salim Abdallah Try Again.

Mo Dewji amethibitisha kukasimisha madaraka yake kwa Try Again kupitia video yake iliyowekwa kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii mapema hii leo Jumatano (Septemba 29).

Mo amewatoa wasiwasi Mashabiki na wanachama wa klabu hiyo kwa kuwaambia kuwa kukasimu madaraka yake kwa kiongozi mwingine wa bodi, hakumaanishi kama yeye anaiacha klabu ya Simba, bali ameamua kujipa muda wa kuendelea na mambo mengine.

Amesema anaipenda na kuithamini klabu hiyo na katu hatoiacha hadi siku anaingia kaburini.

“Kwa mamlaka niliyonayo ninamteua Salim Abdallah Muhene ‘Try again’ kuwa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC.”

“Siondoki Simba, bado nipo Simba na nitaendelea kuwa nanyi, nimeona nikasimu madaraka kwa mwenzangu ili niendelee na majukumu mengine.” amesema Dewji.

Try again aliwahi kuwa Mwenyekiti (Rais) wa Simba SC baada ya sakata la Evance Aveva na amekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi katika kipindi cha miaka 4 ya Uenyekiti wa Mohammed Dewji.

Ujerumani muungano wasubiriwa kwa hamu
Dokii: Viongozi kuweni makini na Manara