Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Maiko Mgombela  amefariki dunia baada ya gari alilokua anaendesha  Toyota HIilux lenye namba za usajili T 840 DQF kugonga kiberenge Cha  treni chenye namba za usajili HDTC4 mali ya shirika la Reli katika makutano ya barabara na reli katika eneo la Kilimahewa Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa Morogoro Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo limetokea majira ya saa sita usiku wa kuamkia Mei 23 mwaka huu  na kwamba kiberege hicho kilikua kinatokea Kilosa kuelekea Morogoro mjini.

Kamanda  Musilimu  amesema katika ajali hiyo wamefanikiwa kuokoa maiti moja ambaye ya mwanaume Maiko Mkombera mmiliki wa gari hiyo na majeruhi mmoja mwanamke aliyefahamika kwa jina la Razia Kassimu ambaye kwa Sasa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro.

Rais Samia kufanya ziara Nchini Ghana
Makata, Naftari waipigia magoti TPLB, TFF