Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki ya mwezi Novemba (Emirates Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month).

Morrison ametajwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo akiwashinda Mshambuliaji kutoka nchini Rwanda Meddie Kagere na Kiungo wa Tanzania Jonas Mkude.

Morrison aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kuonesha kiwango kizuri kwa mwezi Novemba huku akiisaidia Simba SC kuibuka mshindi kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Mshambuliaji Meddie Kagere aliingia kwenye mchakato wa kumsaka mshindi wa mwezi Novemba, kutokana na uwezo wake wa kupachika mabao akiwa na kikosi cha Simba kwa mwezi Novemba, ambapo alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Namungo FC, Ruvu Shooting na Red Arrows.

Upande wa Mkude amekuwa muhimili mkubwa katika safu ya kiungo tangu alipokabidhiwa jukumu hilo, baada ya kuondoka kwa Kocha Didier Gomes, mwezi Novemba alitoa mchango mkubwa katika ushindi wa michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Namungo FC, Ruvu Shooting na Geita Gold huku akisimama imara kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Red Arrows ya Zambia.

Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashabiki kwa mwezi Oktoba (Emirates Aluminium Simba ACP Fans Player of the Month), ilichukuliwa na Kiungo Mshambuliaji Hassan Dilunga ‘HD’.

Edo Kumwembe amsambaza Martin Saanya
Majaliwa: Serikali inaunga mkono tamko lililotolewa na Rais Samia