Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anaonekana kupania kwa hali na mali kujing’oa katika nafasi ya 6 kwenda kilele cha Ligi Kuu ya Uingereza, hali inayomfanya kutoona umuhimu wa yeye na timu yake kusherehekea sikukuu ya Christmas bila kujinoa.

Mourinho ameripotiwa kuamuru wachezaji wote pamoja na wafanyakazi wa timu hiyo kuripoti Old Trafford majira ya saa kumi na nusu jioni siku ya Christmas (Desemba 25), jambo ambalo halijazoeleka.

Katika misimu iliyopita, Manchester Utd iliwahi kufanya mazoezi Carrington siku ya Christmas lakini ilikuwa mapema asubuhi kama inavyokuwa kwa timu nyingine ili kuwapa nafasi wachezaji na wanafanyakazi wengine kusherehekea siku kuu hiyo.

Mtangulizi wa Mourinho, Louis Van Gaal, aliwapa wachezaji wake na wafanyakazi wote nafasi ya kupumzika siku ya Christmas.

Chanzo kimoja kimeiambia SunSports kuwa tangazo hilo la Meneja Mourinho limewakera wachezaji wengi na baadhi ya wafanyakazi ambao wamedai hawakuwahi kusikia kitu kama hicho hata walipokuwa chini ya Fergie (Alex Ferguson).

Huenda Mourinho anataka kuhakikisha anaendeleza ushindi alioupata jana wa 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspur na anaona hakuna haja ya kusherehekea Christmas kwa mbwembwe wakati Ushindi wa Ligi unawapita kando.

Lowassa ajitwisha shida za CUF
Wasichana wawili wa miaka 7 wajilipua kwa mabomu sokoni