Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina amewataka wananchi wa Jimbo la Kisesa Wilayani Meatu mkoani Simiyu kutumia vizuri fedha wanazopata kwa kupitia mauzo ya pamba kununua chakula cha kutosha na kukihifadhi ili kuondokana na uhaba wa chakula.

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwagayi Kata ya Itinje Wilaya ya Meatu, ambapo amesema kuwa uamuzi uliofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli kusimamia ongezeko la bei ya pamba umelenga kuboresha maisha ya wananchi wanyonge waliodhulumiwa kwa miaka mingi.

Amesema kuwa Rais amesimamia msimamo usioyumba katika suala la pamba ambapo kwa sasa bei ya pamba imefikia shilingi 1200 kwa kilo tofauti na hapo awali ambapo wakulima walikuwa wakidhulumiwa kwa kulipwa shilingi 600 kwa kilo.

“Rais Magufuli ameweka msimamo kwamba pamba isinunuliwe chini ya shilingi 1000 na kwamba kampuni itakayoshindwa kununua kwa bei hiyo izuiliwe kununua pamba na kufutiwa usajili wa kutonunua tena zao hilo sehemu yoyote nchini”amesema Mpina.

Aidha, Mpina amewataka wananchi hao kutumia mabadiliko hayo ya bei ya pamba kama fursa ya kuboresha maisha badala ya kutumia vibaya fedha hizo kwa mambo ya anasa ikiwemo kuongeza idadi ya wake.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt. Magufuli imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya wananchi wanyonge na ndio sababu ya kuwekwa msimamo huo kuhusu bei ya pamba.

Mkurugenzi Tume ya Uchaguzi aliyepotea apatikana akiwa amefariki
Kesi ya Malinzi na wenzake yafikia patamu, sasa hatma yao kujulikana