Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina, amesema wanaowabeza Mawaziri wa Rais Magufuli  kwa kuusema kuwa wanamuogopa na kuwa hawawezi kumshauri wamechemsha na wanajidanganya.Ameyasema hayo  jimboni kwake Kisesa alipokuwa kwenye Mkutano wenye lengo la kuelezea mikakati na mipango ya utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)na utatuzi wa Changamoto za Jimbo Hilo.

Mpina alisema kuwa Mawaziri wa Serikali ya awamu ya tano wamekuwa wakibezwa kwa kile kinachonadaiwa kuwa wanamuogopa Rais na hawawezi kumsogelea na kumpa ushauri.

“Naenda kinyume na kauli hiyo kwani hao wanaosema hivyo hawaoni tunachokifanya kuzunguka usiku na mchana kutatua kero za wananchi hii ni katika kutekeleza azima ya chama cha mapinduzi na serikali kwa ujumla ya kuwafikia wanachi na kusikiliza matatizo yao, juzi nilikuwa Kahama, nikaenda Geita na Singida na leo nipo Hapa Mwandoya ningefika vipi huko bila wananchi kuleta shida zao”. Alisema Mpina.

Mpina, aliongeza kuwa Ndege aina ya Bombardier Q400 zilizonunuliwa na serikali pamoja na upanuzi wa barabara akitolea mfano wa Barabara ya Mwenge Jijini Dar es Salaam na Barabara ya Airport ya Mwanza, vyote vimefanyika na bado watu wanabeza bila kuona kama Mawaziri wana Mchango na wanamsaidia Magufuli.

 

Video: Chadema yataja siri tano mafanikio ya Ukuta, Janja ya Maalim Seif hadharani
Dani Alves: Nipo Salama, Sikuvunjika