Mr Blue amefunguka kuhusu sakata lililovuma hivi karibuni mitandaoni akidaiwa kumpigia simu mpenzi wake wa zamani Naj ambaye hivi sasa ni mpenzi wa Barakah Da Prince.

Hit maker huyo wa Mboga saba ameeleza kusikitishwa na habari hizo alizodai zimepikwa na Barakah Da Prince na timu yake kwa lengo la kujipatia ‘kick’ ya wimbo wao mpya unaotarajiwa kutoka hivi karibu. Amesema habari hizo zimehatarisha ndoa yake baada ya kusababisha ugomvi mkubwa kati yake na mkewe.

Mr Blue na Mkewe

Mr Blu na mkewe (katikati)

“Wametengeneza kweli hizo story ili kukikisha nyimbo zao lakini wamenikosea sana kwa sababu wanataka kukosanisha ndoa yangu, mimi nina mke ujue siwezi kumpigia simu mtu niliyemuacha ni kosa kubwa sana,” Mr Blue aliiambia XXL ya Clouds Fm.

Mr Blue ameelza kuwa ulizuka ugomvi kati yake na mkewe na hata kufikia hatua ya kutosemeshana kwa siku mbili ndani ya nyumba, hali iliyomtia hasira na masikitiko.

Hata hivyo, Msanii huyo alisema anampenda Barakah Da Prince kama msanii mwenzake na mdogo wake huku akiufananisha ukubwa wao kwenye muziki kama ‘bajaji’ na ‘meli’ hivyo hawawezi kugongana.

“Siku zote meli haiwezi kugongana na bajaji,” alisema Mr Blue. “Yule namchukulia kama mdogo wangu siwezi kugombana naye. Namshauri na ninampenda… ila kama yeye amefanya, na kama hajafanya, na kama kuna watu wake wamefanya kwa ajili ya kuharibu ndoa yangu waoneshe proof (ushahidi) kwenye mitandao,” aliongeza.

Barakah Da Prince na Naj

Barakah Da Prince na Naj

Hivi karibuni, mrembo Naj alisikika akieleza kuwa amejikuta akiingia katika mgogoro na mpenzi wake, Barakah Da Prince baada ya msanii huyo kushika simu yake na kukuta namba ya simu iliyokuwa imeandikwa jina la kike lakini baada ya kuipiga ilionekana ni namba ya Mr. Blue.

Naj alisema kuwa alii-save namba hiyo kwa jina la kike baada ya kukuta ‘missed-call’. Alisema lengo la kufanya hivyo ilikuwa kuona picha ya mwenye namba hiyo kwenye ‘whatsap’.

Inaelezwa kuwa Barakah Da Prince alipoiona namba hiyo, alisikia sauti ya Blue aliyemwambia ‘ampe mwenye simu’.

Yanga Yaushtukia Uwanja Wa Uhuru, Viongozi Washauriwa Kitaalam
Nyota Ya Joe Hart Yazidi Kufifia, Bravo Akaribia Lango La Etihad Stadium