Idadi ya miamala ya fedha, imetajwa Bungeni hii leo Januari 31, 2023 kuwa ilipanda kutoka Shilingi 349.9 milioni Julai, 2022 hadi kufikia miamala ya Shilingi 410.74 bilioni kwa mwezi Desemba, 2022.

Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Miraji Mtaturu ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya mwaka ya kamati ya Bunge ya Miundombinu Bungeni jijini Dodoma.

Amesema, idadi ya watumiaji wa miamala ya simu pia iliongezeka kutoka milioni 38.40 mwezi Julai hadi milioni 40.95 Desemba 2022 huku akitaka yafanyike marekebisho ya sheria ya Reli kuruhusu sekta binafsi kuwekeza katika kutoa huduma za hitaji hilo.

Aidha, ameitaka Serikali kuongeza fedha ili kukabiliana na ufinyu wa bajeti kwa taasisi zilizo katika Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, kutokana na ukwamishaji wa utekelezaji wa majukumu na miradi mbalimbali nchini.

Afrika iondoe dhana ya kikoloni, kunyonywa: Papa Francis
Jeshi la Polisi linanyooshewa vidole: Rais Samia