Mwigizaji maarufu wa Marekani, Charlie Sheen amemvaa mgombea urais wa Republican, Donald Trump akidai kuwa licha ya kujigamba kuwa na ukwasi mkubwa, alimtapeli kwa kumpa zawadi yenye madini bandia.

Sheen amefunguka katika Graham Norton Show hivi karibuni kuwa awali aliktuana na Trump, wakati yeye akiwa anataka kufunga ndoa na mkewe wa zamani. Alisema kuwa mwanasiasa huyo alimwambia kuwa anataka kumpa zawadi kubwa ya harusi yao na alifanya hivyo papohapo.

“Niligundua Donald Trump anaangalia mkono wangu wenye saa. Akasema, ‘nataka kukupa zawadi ya mapema ya harusi kutoka kwangu na mke wangu Melania’. Kwahiyo akasema ‘hii ni ‘platinum diamond Harry Winston’ huku akifungua mikufu ya vishikizo vya shati (cuff links) na akanipatia,” Sheen alisimulia.

Alisema kuwa miezi michache baadae akiwa amevaa vidani hivyo alivyojua ni vya thamani kubwa vikiwa vimeandikwa ‘Trump’, alikutana na mtaalam wa masuala ya vidani ambaye alimueleza kuwa vilitengenezwa kwa ‘madini feki’.

Wakati Sheen anatoa tuhuma hizo nzito kwa Trump ambaye amekuwa akishambuliwa na wasanii wengi, hali inayofanya wengi kushindwa kuamini yupi anasema kweli, mkewe Melania ni sonara mzuri aliyebobea katika ku-design saa na vidani.

Tanzania kupunguza vifo vya watototo wadogo vitokanavyo na Malaria.
Mpango wa Kihistoria Kuzuia Mauaji kwa Watu Wenye Ualbino Barani Afrika Wazinduliwa