Rapa Hamisi ‘Mwana FA’ Mwinjuma ameuchana mtindo wa muziki kutoka nchini Nigeria ambao hivi unaonekana kuzishika nchi nyingi barani Afrika ikiwemo Tanzania na hata kufunika mitindo ya wazawa.

Akiongea na kipindi cha Ladha 3600 cha E-FM, Mwana FA alionesha kushangazwa na namna ambavyo muziki huo unaonekana kuabudiwa nchini wakati yeye anaona ni takataka tu.

“Tumefikia mahali huu muziki wa Kinaijeria unaabudiwa wakati kiukweli ni ‘shit music’,” mwana FA anakaririwa.

Rapa huyo wa ‘Asanteni kwa Kuja’ amesema kuwa yeye hufanya kazi yake na kuuza mashairi kwa kutumia lugha yake inayoakisi mazingira yanayomzunguka hivyo hana sababu za kukimbilia collabo za nje kwa sasa ingawa anauwezo wa kuzipata nyingi. Alisisitiza kuwa hivi sasa anaangalia zaidi muelekeo wa muziki wake na anapotaka kuupeleka yeye.

Hivi sasa Mwana FA anafanya kazi na mtayarishaji wa muziki ‘Hermy B’ ambaye awali waliingia katika mtafaruki miaka michache baada ya kutengeneza naye ‘hits’ kadhaa ikiwemo ‘Unanijua Unanisikia’. Wimbo wake wa ‘Asantendi kwa Kuja’ aliouachia mwishoni mwa mwaka jana unafanya vizuri sambamba na video yake kubwa.

TFF Kuwachukulia Hatua Kali,Viongozi Na Watumishi Wake
Magufuli aokoa shilingi bilioni 7.5 zinazotafunwa ‘kijanja’