Ndoto za klabu za Uingereza za kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ujerumani pamoja na klabu ya Borussia Dortmund, Ilkay Gundogan zimeyeyushwa na viongozi wa BVB ambao wamefanikisha katika mpango wa ushawishi.

Viongozi wa Borussia Dortmund, kwa kipindi kirefu walikua wakimshawishi Gundogan kusaini mkataba mpya baada ya ule wa sasa kutarajia kufikia kikomo mwezi Julai mwaka 2016.
Gundogan mwenye umri wa miaka 24, amekubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Signal Iduna Park, hadi mwaka 2017.

Klabu za Arsenal na Man Utd zilikua mstari wa mbele katika vita ya kumuwania kiungo huyo baada ya kukaririwa na vyombo vya habari mwezi Aprili kwa kukisema anahitaji kuondoka nchini Ujerumani.
Mipango ya Gundogan ilikua kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya baada ya kuona hali ilikua mbaya katika klabu yake ya Borussia Dortmund, ambayo msimu uliopita haikufanya vyema katika ligi ya nchini Ujerumani.

Klabu ya Borussia Dortmund, ambayo ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa nchini Ujerumani msimu wa 2010-11 kisha 2011-12 ilimaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ya nchini humo msimu uliopita hatua ambayo inaiwezesha kushiriki michuano ya Europa League msimu ujao.

Juventus Waivimbia FC Barcelona Usajili wa Pogba
Mourinho: Sikupingana Na Roman Abramovich kuhusu Petr Cech