Kiungo wa klabu bingwa nchini England Leicester City, N’Golo Kante amewataka viongozi wa klabu za PSG pamoja na Arsenal, kufanya subra katika harakati zao za kutaka kumsajili.

Kiungo huyo ambaye tayari amshaugomea uongozi wa The Foxes kusaini mkataba mpya kwa shinikizo la kutaka kuondoka wakati wa majira ya kiangazi, amewasilisha ujumbe huo kwa wahusika wa Asenal na PSG, kwa kutaka kujipa nafasi ya kuelekeza akili yake kwenye fainali za barani Ulaya (Euro 2016) ambazo zitaanza rasmi Juni 10 nchini Ufaransa.

Amesema haoni sababu ya kuendelea kufuatiliwa huku akifahamu fika anakabiliwa na jukumu zito la kuitetea Ufaransa katika fainali hizo ambazo zinashirikisha zaidi ya mataifa 20.

“Nipo katika maandalizi ya fainali za Euro 2016, kwa hiyo siyapi nafasi masuala ya uhamisho kwa sasa japo najua nini kitakachofuata baada ya kumaliza jukumu nililonalo kwa sasa.

“Mpaka sasa mimi ni mchezaji wa Leicester, na sina nafasi ya kuzunguzia jambo lolote kuhusu usajili.”

Klabu za PSG na Arsenal zimekua zikipigana vikumbo kuiwania saini ya kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, kutokana na kuamini uwezo wake utakua chachu ya kuzisaidia katika msimu wa 2016-17 ambao utaanza rasmi mwezi August.

Hata hivyo Kante aliwahi kuwaeleza baadhi ya rafiki zake wa karibu kuhusu mipango yake ya sasa, ambapo sehemu ya mipango hiyo ni kutohitaji kurejea tena nchini Ufaransa ambapo aliwahi kucheza soka akiwa na klabu ya Caen kabla ya kujiunga na Leicester City mwaka 2015.

Kutokana na mpango huo wa Kante, huenda PSG wakawa na nafasi finyu ya kukamilisha harakati za kumsajili kiungo huyo ambaye tayari amshaitumikia Leicester City katika michezo 37 na kufunga bao moja.

Jose Mourinho Aingiza Figisu Figisu Usajili Wa Mascherano
Kipre Herman Tchetche Aichoka Ligi Ya Bongo