Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo IJUMAA litachezesha droo ya Nusu Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani humo (Uefa Champions League).

Droo hiyo itachezeshwa makao makuu ya Shirikisho la soka barani Ulaya mjini ‘NYON’ nchini Uswiz, na itahudhuriwa watu mashuhuri hasa wanasoka wa zamani pamoja na viongozi wa klabu zilizofuzu hatua ya nusu fainali.

Droo hii itaanza mishale ya saa 8:00 Mchana kwa saa za Afrika Mashariki, na itarushwa Mubashara kupitia Channel SuperSport 3.

Upangaji wa hatua nusu fainali unazihusisha klabu nne ambazo zilifanikiwa kufuzu kwa kushinda michezo ya Robo Fainali.

Klabu hizo ni Real Madrid (Mabingwa watetezi), Atletico Madrid, Juventus na AS Monaco.

Live: Kuaga mwili wa aliyekuwa mbunge, Dkt. Elly Macha Dodoma
Video: Mwakyembe asema ni kazi ngumu kumsafisha Lowassa kuhusu Richmond