Kamati za Bunge za Miundombinu na Hesabu za Serikali (PAC), imetumia usafiri wa njia ya Reli, kufanya safari ya toka jijini Dodoma kuelekea Mkoani Morogoro kwakupitia reli mpya ya kisasa, SGR.

Safari hiyo, inayoongozwa na Mkurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa imeanza hii leo Septemba 26, 2022 kwa lengo la kufanya ukaguzi wa ujenzi wa reli ya mwendo kasi.

Ujenzi wa Reli ya Mwendokasi.

Kabla ya kuanza kwa safari hiyo, mbele ya vyombo vya Habari Kadogosa ameiambia Kamati kuwa, Desemba 2022 treni ya mwendo kasi inaweza kusafiri kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma na ujenzi wake unaendelea vizuri.

Treni ya mwendo mrefu, inapita katika reli hiyo ya mwendo kasi kwa mara ya kwanza ikiwa imebeba Wabunge hao, ambapo pia watapewa taarifa za ujenzi kwa kila kituo hasa vya kupozea umeme.

NASA watoa mwongozo kuiona Jupiter
TRA yashauri somo la kodi Mitaala ya Elimu