Meneja wa Man Utd Jose Mourinho amemwambia kiungo Paul Pogba asahau kuwa nahodha wa kikosi cha Mashetani Wekundu, baada ya kuwaongoza wenzake katika michezo kadhaa tangu kuanza kwa msimu huu wa 2018/19.

Kwa mujibuwa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya The Times, The Telegraph na ESPN, Mourinho amefikia hatua ya kumtamkia Pogba maneno hayo, kufuatia kuchukizwa na kauli aliyoitoa mwishoni mwa juma lililopita, baada ya mchezo wa ligi dhidi ya Wolverhampton Wanderers, ambao limalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.

Pogba alikaririwa na vyombo vya habari akisema, kikosi chao kinapasa kutumia mfumo wa kushambulia wakati wote, kinapokua kwenye uwanja wa nyumbani (Old Trafford), tofauti na walivyocheza katika mchezo huo, na kuambulia matokeo ya sare.

Vyombo hivyo vya habari, vinaamini Mourinho amechukizwa na kauli iliyotolewa na kiungo huyo kutoka nchini Ufaransa, na anaamini nafasi aliyokua nayo ya kuwa nahodha ndiyo ilimpa fursa na kuongea na wanahabari.

Tayari Pogba ameshakiongoza kikosi cha Man Utd kwa nahodha katika michezo mitatu msimu huu, kufuatia kutokuwepo kwa Antonio Valencia. Jana jumanne hakucheza mchezo dhidi ya Derby, huku kitambaa cha unahodha kikikabidhiwa kwa Ashley Young.

Video: Ben Pol aachia ngoma mpya 'Ntala nawe' Monalisa yumo
Vivuko vya Kigamboni kusitishwa, daraja la Nyerere kutumika

Comments

comments