Mwanamuziki mahiri wa muziki wa R&B nchini. Benard Paul maarufu Ben Pol amepata fursa adhimu ya kuwa mmoja wa wanamuziki nyota watakaotumbuiza kwenye jukwaa kubwa la ‘World Youth Forum’.

Licha ya kutumbuiza katika tamasha hilo, Ben pol anatapa nafasi ya kukutana na watu mbali mbali mashuhuri Duniani akiwamo Itziar Ituño maarufu Inspector Murillo, muigizaji mahiri aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia mfululizo wa tamthilia ya ‘Money Heist’.

World Youth Forum, ni jukwaa kubwa la vijana Duniani lenye mlengo wa kuwakutanisha vijana kutoka maeneo tofauti duniani ili kujadili mambo mbali mbali ikiwamo kuhamasisha harakati za kimaendeleo, amani, upendo na umoja, ambalo kwa mwaka huu wa 2022 hafla hiyo itafanyikia huko nchini Misri.

Afisa wa polisi akatisha uhai wake
Rais Kenyata na Raila waungana