Mchekeshaji aliyejizolea umaarufu hivi karibuni, Pierre Liquid ametimiza ahadi yake kwa Mkuu (DC) wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo aliyoitoa tarehe 30 Machi katika harambee ya ‘Kampeni ya Tokomeza Zero’.

Katika kampeni hiyo, Pierre aliahidi kiasi cha shilingi laki moja, lakini amepeleka madawati ishirini yanayozidi thamani ya kiasi cha fedha alichoahidi.

Baada ya kupokea madawati hayo DC Jokate ameandika kwenye mitandao ya kijamii, “Leo nimepokea madawati 20 yenye viwango vya juu kutoka kwa Piere Liquid. Kwenye Harambee yetu ya tarehe 30/03/2019 aliahidi kutoa laki moja lakini leo amekuja na madawati 20 yenye thamani ya zaidi ya Tsh. laki moja. Kwa niaba ya WanaKisarawe nasema asante sana kwa mchango wako bado ahadi ya kutengeneza madawati na hii kampuni inabaki. Asante.”

Machi 31, 2019 Piere aliahidiwa na Jokate kupewa tenda ya kutengeneza madawati katika shule inayotarajiwa kujengwa wilayani humo.

Zitto afunguka unyanyasaji kuhusu uraia mipakani, Serikali yampa heko
Video: JPM atoa agizo baada ya kupokea gawio kutoka TTCL

Comments

comments