Siku moja baada ya Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuridhia barua ya ombi la kuwavua Ubunge wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF), Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba ametangaza kuanza kuwahoji wabunge wa majimbo kwakosa la kukihujumu chama

Amesema  kuwa Kamati ya Maadili na Nidhamu ya chama hicho imeanza na wabunge nane wa viti maalamu na madiwani wawili, hivyo awamu ya pili, watahojiwa wabunge wa majimbo pamoja na Maalim Seif ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho pamoja na wanachama wengine

Aidha, Wabunge 8 wa CUF waliovuliwa ubunge ni wabunge wa viti maalum wa chama hicho, na tayari  Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imeteuwa wabunge wanane wa Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuiarifu tume kuwepo kwa nafasi hizo, kufuatiwa kutenguliwa kwa ubunge wa wabunge waliokuwa wanashikilia nafasi hizo

Hata hivyo, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kailima imewataja wabunge hao kuwa ni, Rukia Ahmed Kassim, Shamsia Aziz Ntamba, Kizza Hussein Mayeye, Zainabu Mndolwa Amir, Hindu Hamis Mwenda, Sonia Juma Magogo, Afredina Apolinary Kahigi, na Nuru Awadhi Bafadhil

Mbowe amjibu Polepole kuhusu kigogo wa Chadema anayetarajiwa kuhamia CCM
Video: Spika akata, NEC yafunua, Tutanyamaza tukiwa wafu - Lissu