Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof. Kitila Mkumbo amepongeza hatua zilizochukuliwa na kiongozi wa muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), Raila Odinga za kwenda mahakamani kudai haki yake.

Amesema kuwa kipindi ambacho kina Odinga wanapambana kupigania mageuzi wakati wa muhula wa pili wa utawala wa Rais Daniel Arap Moi, Uhuru Kenyatta yeye alikuwa kivulini

Prof. Mkumba amesema kuwa Raila Odinga ni mwanasiasa aliyekomaa kidemokrasia hivyo anafaa kuitwa baba wa demokrasia barani Afrika huku akiwataka wanasiasa kuiga mfano huo.

“Ahsante sana Raila Odinga kwa hakika maamuzi uliyofanya kwenda mahakamani kutafuta haki ni maamuzi sahihi, wewe ni baba wa Demokrasia katika ukanda huu,”amesema Prof. Mkumba

Hata hivyo, uchaguzi mkuu nchini Kenya umefanyika hivi karibuni ambapo mgombea kutoka chama tawala cha Jubilee, Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi na kumbwaga Raila Oadinga kuthoka ODM.

 

Mkasa: Waliniambia nina roho ya Paka mbona sifi, nilipigwa kuanzia saa 4 - 12 (Video)
Mkemia Mkuu awanyooshea kidole mawakala wa forodha