Wadau wa habari wametakiwa kujiaanda na utoaji wa hoja za utetezi wa hitaji lao la marekebisho ya baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma za Habari 2016.

Wito huo umetolewa na Mbunge wa Ubungo (CCM), Profesa Kitila Mkumbo ambaye amesema mara baada ya kuitwa kwenye kamati ni vyema Wanahabari hao wakawa na hoja za ushawishi ili kufanikisha jambo hilo.

Amesema, “Kwenye kamati ndio wadau wanapata nafasi ya kutoa hoja zao kwanini wanataka baadhi ya vipengele vifanyiwe marekebisho, sasa vi vyema kujiandaa na hilo.”

Suala hili la mabadiliko ya sheria ya Habari, limekuwa likizungumziwa tofauti na wadau akiwemo Mbunge wa Nanyamba (CCM), Abdallah Chikota ambaye anasema hawezi kuzungumzia chochote hadi hapo atakapouona muswada wa marekebisho hayo.

Chikota, ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii anaongeza kuwa, “Ukija basi tutaangalia marekebisho gani yaliyopo na kuuchambua kama utaletwa katika kamati yetu.”

Napema hivi karibuni, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile alisema mpaka sasa hawajajua ni lini marekebisho hayo yatapelekwa bungeni, lakini wanaamini Serikali tarai imeonyesha nia ya kufanya mabadiliko.

TRA yashauri somo la kodi Mitaala ya Elimu
Al Hilal kuweka kambi DR Congo