Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amemu-unfollow  kwenye mtandao wa Twitter mwimbaji maarufu nchini humo, Jose Chameleon muda mfupi baada ya mwimbaji huyo kutangaza nia ya kugombea Umeya wa jiji la Kampala mwaka 2021.

Chameleon ametangaza kujiunga na chama cha siasa cha Democratic Party (DP) ili afanikishe nia yake ya kuwa Meya na kuwatumikia wananchi.

Ametangaza uamuzi huo leo katika uwanja wa mpira wa Kakindu uliopo katika mji wa Jinja.

Rais Museveni amekuwa akiwafuata watu 24 tu kwenye mtandao wa Twitter. Kati yao kulikuwa na wasanii wawili pekee ambao ni Chameleon na Bebe Cool.

Jose Chameleon

Awali, Chameleon alikuwa mmoja kati ya wasanii waliohusika kufanya wimbo wa ‘Tubonge’ ambao ulitumika kama wimbo wa kampeni wa Rais Museveni katika uchaguzi uliopita. Pia, alikuwa mmoja kati ya wasanii waliokuwa wanatumbuiza kwenye jukwaa la kampeni la Museveni.

Chameleon amefuata nyayo za Bobi Wine ambaye hivi sasa ni mbunge na mpinzani mkubwa wa Serikali ya Museveni.

TRA waonywa, 'Msiwasumbue wafanyabiashara'
Biteko apangua hoja ya dhahabu Kigoma. 'Hii si sahihi hata kidogo'

Comments

comments