Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amesema kuwa maadhimisho kuelekea siku ya Ukimwi duniani yatafunguliwa Novemba 24, 2021 na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson katika viwanja vya Ruanda – Nzovwe jijini Mbeya.

Akizungumza na waandishi wa habari RC Homera amesema Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani yanayofikia kilele chake Desemba Mosi mwaka huu mkoani Mbeya.

Ameongeza kuwa, pia kutakuwa na kongamano la vijana ikiwa ni maandalizi ya kuelekekea siku ya Ukimwi duniani.
 
Siku ya Ukimwi duniani huadhimishwa Desemba mosi ya kila mwaka ambapo Wanaharakati na Wakuu wa nchi hutumia siku hiyo kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vinavyosababisha ukimwi, kupiga vita unyanyapaa na kuhimiza watu kwenda kufanya vipimo ili kufahamu hali zao.

Wanaouza Damu dawa inachemka
Try Again: Tutamsajili yoyote, fedha tunayo