Rais wa Pakistan, Mamnoon Hussain ametangaza kuzifuta nchini kwake shamrashamra na sherehe za siku ya wapendanao duniani, Valentine’s Day, Februari 14.

Rais Hussain ameeleza kuwa ameamua kuipiga marufuku sikukuu hiyo kwa kuwa ni utamaduni wa ‘Magharibi’ na haina uhusiano wowote na utamaduni wa Pakistan.

Aliwaambia wanafunzi wa nchi hiyo kuwa wanapaswa kufahamu Valentine’s Day ni sherehe ya Ki-Magharibi na kwamba inakinzana na imani ya Kiislam hivyo hawapaswi kuungana nayo.

Rais huyo ameagiza Jeshi la polisi kutembelea maduka yote madogo kwa makubwa kuangalia kama kuna mtu anauza kadi, maua au vitu vinavyoashiria sikukuu ya Valentine ili achukuliwe hatua.

Barua ya Pakistan

Hivi karibuni, Uongozi wa jiji la Banda Aceh la Indonesia ulitangaza hatua kama hiyo.

Valentine burned

Sababu 3 muhimu, Kwanini hupaswi kufanya ngono siku ya Valentine
Serikali Ya Magufuli kusambaza madaktari Bingwa 'Pembezoni'