Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Modestus Francis Kipilimba alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Dkt. Modestus Francis Kipilimba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Rashid Othman ambaye amestaafu katika nafasi hiyo.
Aidha katika hatua nyingine Rais Magufuli amemteua Bw. Robert Msalika kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Idara hiyo ya Usalama wa Taifa.
                                                                                                                                      Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. George Madafa kuwa Balozi na nchi atakayopangiwa itatajwa baadaye.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Atoa Neno Kuhusu Mamilioni Ya Raisi Magufuli
Hospitali Ya Siha Mkoa Wa Kilimanjaro Watatua Tatizo La Dawa