Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali, Marco E. Gaguti ametekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli la kugawa vitambulisho kwa Wajasiliamli Wadogo ili waweze kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato bila kusumbuliwa na mtu yeyote.
 
Ametekeleza agizo hilo la kugawa vitambulisho hivyo katika Manispaa ya Bukoba ambapo amevigawa kwa Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa wa Kagera na Halmashauri zake nane.
 
Akizungumza na Wakuu hao wa wilaya kabla ya kuvigawa, amesema kuwa Mkoa wa Kagera ulipewa vitambulisho 25,000 vilivyotolewa na Rais Magufuli na kusisitiza kuwa vitambulisho hivyo vikigawiwa na kuisha uongozi wa mkoa utaomba vingine zaidi ili kuhakikisha kila Mjasiliamali Mdogo anapata kitambulisho hicho.
 
”Rais Magufuli alitoa maelekezo kuwa hakuna Mjasiliamali yeyote ambaye atakuwa na kitambulisho na kusumbuliwa, pia na mimi narudia na kuagiza kuwa Mjasiliamali Mdogo yeyote ambaye atakuwa na kitambulisho na kusumbuliwa na mtu yeyote katika mipaka ya Mkoa wa Kagera.” Amesema Gaguti
 
Aidha, amewatahadharisha wafanyabiasha wadanganyifu kuwa tayari ofisi yake imepata taarifa kuwa kuna baadhi ya Wafanyabiashara wasio waaminifu na kwamba wameanza kupunguza bidhaa kwenye chanja za maduka yao ili waweze kutambuliwa kama Wajasiliamali Wadogo wakilenga kupata vitambulisho.
 
Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kagera, Adam Ntoga amesema kuwa ni Wajasiliamali wadogo wadogo ambao hawajawahi kutambuliwa na mfumo wa kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na mzunguko wao wa fedha haufikii kiasi cha shilingi milioni nne, huku akiongeza kuwa malipo ya kitambulisho hicho ni shilingi 20,000/- tu.
 
Katika Mkoa wa Kagera Wilaya ya Bukoba ilipatiwa jumla ya vitambulisho 3,580 na Wilaya za Missenyi, Karagwe, Kyerwa, Ngara, Biharamulo na Muleba kila Wilaya kupitia Wakuu wa Wilaya zilipatiwa vitambulisho 3,570 na kukamilisha jumla ya Vitambulisho 25,000 vilivyotolewa katika Mkoa wa Kagera na Rais Magufuli Disemba 10, 2018.
 
  • Maporomoko ya Mto Ruhuji kuanza kuzalisha umeme
  • Makonda anena makubwa mbele ya JPM, ‘2020 kitaeleweka tu’
  • LIVE: Rais Magufuli akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa daraja jipya la Salenda
 
Hata hivyo, Disemba 10, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika JICC Jijini Dar es Salaam alitoa vitambulisho vya wajasiliamali wadogo 670,000 kwa Wakuu wa Mikoa yote na kila Mkoa ulipatiwa vitambulisho 25,000 na Mkoa wa Kagera ukiwemo ambapo Rais Magufuli alisema kuwa kila Mkuu wa Mkoa atakusanya shilingi 500 milioni kupitia vitambulisho hivyo
Mchomvu awapiga dongo Wasafi... ‘msiwe mnatucheka, mjifunze’
Maporomoko ya Mto Ruhuji kuanza kuzalisha umeme

Comments

comments