Meneja wa klabu ya Southampton, Ronald Koeman amewapa masharti viongozi wa klabu hiyo ili kufanikisha azma ya kusiani mkataba wa kuendelea kufanya kazi klabuni hapo.

Koeman aliwahi kuripotiwa kuwa njiani kukamilisha mpango wa kusaini mkataba mpya kutokana na mazungumzo kati yake na mabosi wa The Saint kwenda vyema, lakini imeonekana kuna walakini katika baadhi ya mambo, hivyo ameomba kuhakikishiwa kwanza.

Jambo kubwa ambalo limekuwa kikwazo cha kukamilika kwa mpango wa kusainiwa kwa mkataba wa pande hizo mbili, ni uhakika wa kutengwa kwa fungu la usajili wa wachezaji ambao watakidhi haja ya meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.

Koeman, anataka kuhakikisha jambo hilo ambalo kwake anaamini litakua la msingi, kabla ya kufanya maamuzi ya kujitia kitanzi cha kusaini mkataba mpya.

Hata hivyo tayari mlinda mlango wa The Saint, Fraser Forster, beki Virgil van Dijk pamoja na kiungo James Ward-Prowse wameshakubali kusaini mikataba na Koeman alionekana kuwa mstari wa mbele kuwapigania wachezaji hao kubaki klabuni hapo.

Lakini hali kama hilo imekua ngumu kwa mshambuliaji Shane Long ambaye anapigiwa hesabu za kusajiliwa na klabu ya Liverpool pamoja na mabingwa wa nchini England The Foxes.

Kwa upande wa mshambuliaji Sadio Mane naye anatajwa kuwa kwenye harakati za kuondoka klabuni hapo kufuatia ofa kadhaa kuendelea kuwasili.

Chid Benz atoroka Rehab, Meneja wa kituo aeleza kilichomkuta
Antonio Conte Amuweka Njia Panda Alexandre Pato