Shirika la Ndege Precision Air, limeanza safari za moja kwa moja kutoka jijini Dar-es-salaam na Zanzibar kwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ili kuongeza kipato kinachotoka kwenye sekta ya utalii na kuboresha miundombinu ili kukuza idadi ya watalii.

Meneja mahusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete, alisema kuanzishwa kwa safari hizo kutapunguza adha ya usafiri kwa watalii wanaopenda kutembelea hifadhi hiyo. Hivyo alitoa shukrani za dhati kwa Shirika la Ndege Precision Air na wadau wengine kwa kuliangalia jicho la tatu swala la utalii wa ndani.

Uzinduzi huo ulifanyika katika uwanja mdogo wa Seronera, uliopo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti, amabao utaongeza ufanisi katika kukabiliana na changamoto ya miundombinu inayozuia idadi kubwa ya watalii kutotembelea vivutio hivyo.

#HapoKale
Diamond na Ommy watoleana povu, Ommy Dimpoz adai amejipanga.