Mshambuliaji kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati Cesar Lobi Manzoki, ameipongeza Simba SC, kwa kufanikisha Tamasha la Simba Day jana Jumatatu (Agosti 08), Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam.

Manzoki ambaye anahusishwa na usajili wa Simba SC, ametoa pongezi hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuweka picha ya pamoja ya wachezaji na Benchi la Ufundi iliyopigwa baada ya kutambulishwa katika Tamasha hilo.

Manzoki ameandika: Hongera @simbasctanzania kwa kufanikisha hili, ilikua siku nzuri kwa Mashabiki wa Simba, ninakubali klabu hii ni kubwa Barani Afrika.

Mshambuliaji huyo alikuja Dar es salaam akiwa na kikosi cha Klabu yake ya Vipers SC ya Uganda, kwa ajili ya mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya Young Africans katika Kilele cha Wiki Wananchi Jumamosi (Agosti 06).

Mchezo huo ulimalizika kwa Vipers SC kushinda 2-0, huku Manzoki akiwekwa Benchi.

Dili la Manzoki kujiunga na Simba SC linatajwa KUFELI kutokana na Uongozi wa Vipers SC kuhitaji kiasi kikubwa cha pesa ili kuvunjwa kwa mkataba wake uliosaliwa na muda wa miezi miwili.

Kenya: Martha Karua abadilishiwa kituo cha upigaji kura
'Biometric' yashindwa kumtambua mgombea Urais Kenya, wasiwasi waibuka