Meneja msaidizi wa klabu ya Chelsea Steve Holland, ameteuliwa kuwa msaidizi wa kocha mkuu wa timu ya taifa ya England  Gareth Southgate.

Chama cha soka nchini England (FA) kimethibitisha uteuzi wa Holland ambaye aliwahi kufanya kazi na klabu ya Crewe Alexandra kuanzia mwaka 2007 hadi 2008 na baadae alipata ajira ya kuwa kocha wa kikosi cha wachezaji wa akiba wa Chelsea kuanzia mwaka 2009 hadi 2011.

FA wamesisitiza kuwa Holland ataanza kazi mara moja, na atasaini mkataba wa kuitumikia timu ya taifa ya England jumla, ili kutoa nafasi ya kusaidiana kwa uhakika na bosi wake Southgate.

Wawili hao waliwahi kufanya kazi katika kikosi cha timu ya taifa ya England chini ya umri wa miaka 21, hivyo inaaminiwa watafanikiwa kuleta mabadiliko.

Shahidi wa pili atoa ushahidi kumbana Lissu, akumbana na swali la Kibatala
Msongo Wa Mawazo Wamvuruga Alexis Sanchez