Wanamgambo wa Taliban wametoa tamko kwa serikali ya Marekani kuwa hawatatangaza Serikali mpya mpaka Marekani itakapo kamilisha kuviondoa vikosi vyake nchini Afghanistan.

Hayo yamesemwa na mfuasi wa Taliban Muhammad Suhail Shaheen katika ofisi mojawapo iliyopo mji wa Duha nchini Qatar .

Hatua hii imejiri baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza kuongeza muda wa vikosi vya Marekani kuwepo nchini humo mpaka Agosti 31 mwaka huu, Kundi hilo limeonya kwamba halitakubali Marekani kurefusha muda wa mwisho wa Agosti 31 wa kuyaondoa majeshi yake na kuonya kwamba kufanya hivyo kutakuwa na athari kubwa.

Wakati huohuo msemaji wa muda mrefu wa kundi la Taliban Zabihullah Mujahid, amewataka Maimamu nchini humo kuwapa uhakikisho Waafghanistan juu ya usalama wao na kuondoa propaganda zisizo na misingi zinazoenezwa na Marekani juu ya Taliban.

Wanne wajeruhiwa ajali ya basi la Sauli
Malengo ya Wizara ya Madini kukusanya Bilioni 650