Zikiwa zimebaki siku nne laini za simu zisizosajiliwa kwa alama za vidole kufungiwa, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaagiza Watanzania waliokamilisha usajili wa laini zao kuhakiki upya kwa kupiga namba *106#.

“Kama mnavyofahamu, mwisho wa kutumika kwa laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa kutumia namba ya kitambulisho cha taifa (Nida) na kuthibitishwa kwa alama za vidole ni Januari,20, 2020, kama umeshasajili hakiki tena usajili wa laini zako kwa kupiga namba *106# na uchukue hatua stahiki sasa,” imeeleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imetolewa rasmi leo January 16, 2020 na Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba kwa watu wote ambao bado hawajasajili laini zao za simu na kuwataka kutumia siku hizi nne zilizobaki kukamilisha usajili huo ili kuepuka adha itakayojitokeza mara baada ya laini kufungwa.

Pia amesema zoezi la usajili wa simu litakuwa endelevu hata kwa wale ambao watakuwa wamefungiwa wataweza kufungua laini zao kwa kuzisajili, lakini pia kwa wale ambao watanunua laini mpya pia wataweza kusajili laini hizo.

“Kwa watakaositishiwa huduma za laini zao za simu Januari 20 wanaweza pia kuendelea na utaratibu wa usajili kwa lengo la ama kurudisha laini zao zitakazokuwa zimefungwa au kupata laini mpya,”.

“Kwa watumiaji/waombaji wapya wa laini za simu wataendelea kusajiliwa muda wote na usajili huo kwa kutumia kitambulisho cha taifa na kuhakikiwa kwa alama za vidole, huduma ambayo ni endelevu pia.”

Pia ameongezea kuwa kwa wanadiplomasia au taasisi ambao hawajakamilisha usajili wa laini   za simu au zinazotumika kwenye vifaa vyao vya mawasiliano waendelee kufuata utaratibu waliowekewa.

Aidha zoezi la usajili kwa alama za vidole ni moja ya zoezi linalochukua muda mfupi usiozidi dakika tano  kuliko matarajio ya watu wengi ambao wanadhani kuwa zoezi hilo linatumia muda mwingi kama ilivyo mazoezi mengine kama vile kurudisha line iliyoptea, zaidi tu kuhakikisha una namba yako ya NIDA au kitambulisho chako cha NODA ili kukamilisha usajili huo.

Hivyo nitumie nafasi hii kwa wewe utakaye bahatika kusoma taarifa hii kama bado hujasajili line yako na un akitambulisho cha taifa, tafadhali fika katika ofisi husika zinazofanya usajili uweze kusajili ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza mara baada ya line yako kufungwa.

 

Video: Twiga anawakilisha nini kwenye nembo ya taifa, sikiliza hapa majibu ya watu
Lukuvi atumbua jipu: Benki zinavyotumia madalali kutapeli nyumba Dar

Comments

comments