Mama mzazi wa mshereheshaji Emmanuel Matebe maarufu kama MC Pilipili, Mariam Matebe amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 20, 2020, kwa ajali ya gari wakati akielekea ukumbini kwenye harusi ya mtoto wake maeneo ya Afrikana Jijini Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram MC Pilipili ameandika, “Ulale salama mama yangu mpenzi Mariam Matebe, umetufundisha upendo na umefariki ukijariibu kuonesha upendo lala salama mpenzi”.

Ujumbe ulioambatana na picha za mwisho walizopiga muda mfupi baada ya mdogo wake wa kiume Thomas Matebe kufunga ndoa jana mchana Desemba 19.

Kwa mujibu wa familia mwili wa marehemu wa mama mzazi wa MC Pilipili  utasafirishwa leo jioni kuelekea nyumbani kwa marehemu Jijini Dodoma kwa ajili ya taratibu za maziko.

RC Kunenge awaonya madalali
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Desemba 20, 2020