Mshambuliaji wa Nigeria Odion Ighalo 30, ametoa ombi la kibinafsi kwa klabu ya china ya Shanghai Shenhua, la kutaka kurefusha mkataba wake wa mkopo Manchester United. (Manchester Evening News)

  • Liverpool wanataka kumsaini winga wa Wolves na Hispania Adama Traore, 24, huku mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp akiripotiwa kuwasiliana na mchezaji huyo moja kwa moja. (TodoFichajes – in Spanish)
  • Muda wa David Luiz Arsenal unaelekea kukamilika baada ya kubainika mkataba wa kiungo huyo wa Brazil wa miaka 33 unakamilika mwezi ujao. Mpaka sasa hakuna mazungumzo yoyote yaliyoanzishwa kuhusu mkataba mpya. (Sky Sports)
  • Liverpool haitalipa ada ya £50m itakayomwezesha mshambuliaji wa RB Leipzig na Ujerumani Timo Werner 24, kujiunga nao wakikadiria kuwa thamani yake ni £30m katika soko la sasa la uhamisho. (Mirror)
  • Beki wa Ajax na Argentina Nicolas Tagliafico 27, huenda akajiunga na Chelsea kwa ada ya £22.4m. (Telegraph – subscription required)
  • Tottenham wanapania kuwapiku washindani wao kadhaa wa Ligi Kuu England katika usajili wa winga wa Bournemouth na Scotland Ryan Fraser, 26. (Football Insider)
  • Beki wa Newcastle Mhispania Javier Manquillo 26, anataka kujiunga na klabu ya La Liga club nchini kwao mkataba wake utakapo kamilika mwezi ujao. (Newcastle Chronicle)
  • Manchester United na Real Madrid wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Rennes Ufaransa Eduardo Camavinga, 17. (Metro)
  • Mkufunzi wa Tottenham Jose Mourinho klabu hiyo haitatumia fedha nyingi awamu ijayo ya uhamisho wa wachezaji. (Sky Sports)
ASFC: Azam FC mdomoni mwa Simba SC
Chama cha madaktari kufanya uchambuzi wa nyungu kupunguza Corona