Beki kutoka nchini Ubelgiji na klabu ya FC Barcelona, Thomas Vermaelen huenda akawa sehemu ya kikosi cha klabu hiyo katika michezo miwili iliyosalia kwa msimu huu.

Vermaelen anapewa nafasi kubwa ya kuwa sehemu ya kikosi cha FC Barcelona mwishoni mwa juma hili katika mchezo wa ligi na kisha mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la Mfalme, kutokana na kupona jeraha la kiazi cha mguu ambalo lilikua likimsumbua tangu April 11 mwaka huu.

Jana beki huyo, ameripotiwa kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha FC Barceklona na tayari meneja Luis Enrique ameonyesha kuridhishwa na mwenendo wake, hivyo huenda akamtumia katika mpambano wa ligi wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Granada.

Katika mchezo huo, Barca itawalazimu kushinda, ili wafanikishe azma ya kutetea ubingwa wao wa La Liga, na kama watashindwa kufanya hivyo na mpinzani wao wa karibu Real Madrid akafanikiwa kuwafunga Deportivo La Coruna mambo yatawaharibikia.

Vermaelen ambaye alisajiliwa na FC Barcelona akitokea Arsenal, amecheza michezo 20 tangu alipoelekea Camp Nou mwaka 2014, na mara kadhaa amekua akisumbuliwa na majeraha.

John Terry Awekwa Njia Panda, Mkataba Wake Kumalizika Mwezi Ujao
Magufuli atangaza vita na watu 10, asema wakisimama utasikia 'CCM Oyee'

Comments

comments