Kiungo wa klabu bingwa barani Ulaya (Real Madrid) Toni Kroos ametemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ujerumani kufuatia majeraha ya kidole cha mguu alioyapata wakati wa mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Leganes.

Taarifa zilizotolewa na klabu ya Real Madrid zimeeleza kuwa, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, amevunjika mfupa wa kidole cha pili cha mguu wake wa kulia (Metatarsal) na huenda ikamchukua muda wa majuma sita hadi manane ili kurejea tena uwanjani.

Kufuatia majeraha hayo, Kroos ataukosa mchezo wa ligi ya nchini Hispania utaofuata ambapo Real Madrid watapambana na mahasimu wao wa mjini Madrid, Atletico Madrid utakaounguruma Novemba 19 katika uwanja wa Vicente Calderón.

Michezo mingine ambayo Kroos ataikosa kwa upande wa klabu yake ni dhidi ya Sporting Gijon, FC Barcelona, Deportivo La Coruña, Valencia, Granada CF na Sevilla CF.

Kwa upande wa timu ya taifa ya Ujerumani atakosa michezo ya kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya San Marino pamoja na Italia.

Rais Magufuli ampongeza Trump kwa ushindi, amhakikishia hili
Alexis Sanchez Hatarini Kuikosa Man Utd