Rais wa Marekani Donald Trump ametupiwa lawama baada ya kutuma video mtandaoni inayoonyesha mmoja wa wafuasi wake akipaza sauti na kusema “nguvu ya wazungu”.

Imeelezwa kuwa mfuasi wake huyo alikua miongoni mwa kikundi cha watu waliokua wakishiriki mkutano wa kampeni ya uchaguzi ya Bwana Trump katika makazi ya kustaafu yaliyoko Florida.

Trump amekanusha shutuma kwamba anataka kupata umaarufu kupitia hali ya wasi wasi iliyopo kutokana na ubaguzi wa rangi nchini humo . Msemaji wake anasema hakusikia maneno “white power” katika video.

Video hiyo ambayo ilifutwa baadae, iliyowekwa katika ujumbe wa ilimuonyesha mfuasi wa Trump akiwa katika uwanja wa gofu huku akipaza sauti na kusema “nguvu ya wazungu “. Alionekana kuwa alikua akimjibu muandamanaji mwenzake aliyemuita mbaguzi wa rangi na kutumia maneno yasiyo ya staha. 

Rais Trump aliwali alikabiliwa na shutuma za kushirikisha na kunadi kauli za ubaguzi . Mwaka 2017 alituma video tatu za matusi kutoka kwa kikundi cha Uingereza cha mrengo wa kulia, na kusababisha aliyekua Waziri Mkuu wa uingereza wakati huo Theresa May kujibu.

JPM atoa siku saba kufutwa hati za mmiliki wa ardhi asiye mtanzania
Waziri Kalemani Atoa Siku 7 wananchi Mwanza kuwekewa Umeme