Mbunge wa Dodoma Mjini, Anthony Mavunde ameridhishwa na kasi ya usimikaji nguzo katika Kata hiyo na kumtaka Mkandarasi kukamilisha maeneo yaliyobaki ya Mtaa wa Makulu na Mwegamile ili ifikapo Juni,2022 eneo lote liwe limewashwa umeme.

Mavunde ameyasema hayo alipotembelea mradi huo akiambatana na diwani wa kata ya Mbalawala Charles Ngh’ambi katika kukagua mradi huo unaotekelezwa na Kampuni ya Umeme ya Ceylex chini ya mradi wa PERI URBAN.

Naye diwani wa kata ya Mbalawala Charles Ngh’ambi ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu, kwa kasi ya utekelezaji wa mradi huo wa umeme na kuahidi kushirikiana na mkandarasi ili kazi ya usambazaji umeme ikamilike mapema na wananchi waweza kutumia nishati hiyo kwa matumizi ya kiuchumi na kijamii.

Watu watano wajeruhiwa ajali ya basi Tabora.
Wanaotumika kumchafua Mkuu wa Majeshi waonywa