Chama kikuu cha upinzani nchini Angola (UNITA) kimeitisha maandamano baada ya Mahakama ya kikatiba kutupilia mbali kesi yao ya kupinga ushindi wa rais Joao Lourenco, baada ya uchaguzi wa Agosti 28.

Mahakama hiyo katika uamuzi wake imesema aliyekuwa mgombea mkuu Adalberto Costa Junior kutoka chama cha UNITA hakuwasilisha ushahidi wa kutosha, kubadilisha matokeo yaliyompa ushindi rais Lourenco, aliyetangazwa mshindi ili kuongoza nchi hiyo kwa muhula wa pili. 

Matokeo ambayo yalitolewa na tume ya uchaguzi nchini humo yalionyesha chama tawala cha MPLA kiliibuka na ushindi wa asilimia 51.17 na Rais Joao Lourenco kujihakikishia muhula wa pili wa Uongozi huku UNITA ikipata asilimia 43.95 ya kura zilizopigwa.

Adalberto Costa Junior, alikataa kukubali matokeo na kudai kulikuwa na wizi wa kura na hivyo kuamua kwenda kuupinga ushindi wa rais Joao Lourenco, Mahakamani. 

Uamuzi wa Mahakama sasa unatoa nafasi kwa rais Lourenco, kuapishwa wiki ijayo ikiwa wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanahofia kuwa uamuzi huo unaweza kuchochea maandamano miongoni mwa vijana maskini ambao walipigia kura chama cha UNITA.

Serikali ya nchini hiyo imeweka tayari vikosi vyake vya usalama ili kuzuia matukio yanayoweza kuleta usumbufu nchini humo.

Chala tawala cha MPLA kimekuwa madarakani nchini Angola tangu nchi hiyo ilipopata uhuru mwaka 1975.

Polisi watuhumiwa kwa rushwa mpakani
Huduma uokozi wa Maisha zahitaji Dola Mil. 68