Rais Vladimir Putin wa Urusi amesema kuwa hatalipiza kisasi baada ya kufukuzwa wanadiplomasia wake 35 na Marekani kwa tuhuma za kuhusika na udukuzi kwenye uchaguzi wa rais nchini Marekani.

Aidha, Putin amesema atazingatia hatua zitakazochukuliwa na rais mteule Donald Trump anayetarajia kukabidhiwa hatamu ya uongozi january 20 mwakani, kabla ya kuchukua hatua zaidi kuhusu uhusiano kati ya Urusi na Marekani.

Hata hivyo, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi Sergei Lavrow alimshauri rais Putin aamuru Serikali ya mjini Moscow iwafukuze wanadiplomasia 35 wa Marekani na kuwazuia wanadiplomasia hao wa Marekani kutumia majengo mawili yaliyopo mjini Moscow.

Putin amekataa pendekezo la Waziri wake wa Mambo ya Nchi za Nje kwa kusema kuwa hatutomfukuza mtu yeyote.

Vilevile, Putin ameongeza kuwa anaviangalia vikwazo hivyo kwa kina zaidi kwani vinaweza kuvuruga uhusiano kati ya Moscow na Washington na kuongeza kuwa anasikitika sana kuona Serikali ya Obama inamaliza muda wake huku wakiwa katika mkwaruzano.

Wastara aaga mwaka na ujumbe mzito '' hakuna kitu kibaya kama kupoteza furaha na tumaini''
Umri mzuri kwa mwanamke kupata mtoto (kuzaa)