Timu ya Taifa ya Algeria jana ilizima ndoto za Taifa Stars kuwa katika orodha ya timu zitakazowania Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi baada ya kuituliza kwa goli 7-0, idadi ambayo imewatesa mashabiki wa soka nchini.

Algeria ambao wako katika nafasi ya pili hivi sasa kwa ubora wa soka Afrika kwa mujibu wa FIFA, waliutawala mchezo huku Taifa Stars ikizawadiwa kadi za njano zilizozaa kadi moja nyekundu na hivyo kuipunguzia nguvu zaidi.

Waarabu hao walimnyima raha kocha mzawa Boniface Mkwasa kwa jinsi walivyoendelea kuonesha kiu ya kutupia magoli licha ya kuwa na idadi kubwa ya magoli.

Kutokana na matokeo hayo, Stars imeondolewa kwa jumla ya magoli 9-2 katika michezo miwili ya nyumbani na ugenini, katika mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam Stars iliweza kupimana nguvu na Algeria 2-2.

 Kipigo cha cha Taifa Stars ni sehemu ya mpira wa miguu inayowakumbusha wapenzi wa soka kipigo kinachofanana na hicho (7-1), ilichokipokea Brazil kutoka kwa Ujerumani katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana.

 

Urusi, Ufaransa Waivuruga ISIS, Washusha Mabomu Ya Kihistoria
Bunge Laanza Moto, Nape Aambiwa Anasumbuliwa Na Utoto