Kufuatia kifo cha mmoja wa waasisi na mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba, familia yake imetoa rasmi ratiba ya taratibu za mazishi.

Familia hiyo imesema kuwa mwili wa Marehemu unatarajiwa kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa jioni kutokea nchini Afrika Kusini kisha utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam kabla ya kusafirishwa kwenda mkoani Kagera kwa mazishi.

Taarifa hizo zimeeleza kuwa mwili wa Ruge Mutahaba utasafirishwa siku ya Jumapili kuelekea Bukoba mkoani Kagera kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika siku ya Jumatatu.

Ruge Mutahaba amefariki dunia juzi akiwa hospitalini nchini Afrika Kusini alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na tatizo la figo.

Mungu amrehemu.

DCB yatakiwa kuwajengea uwezo wateja wake
Breaking: Mkutano wa Trump na Kim Jong Un wavunjika

Comments

comments