Mbunge wa Jimbo la Busega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji, Dkt. Raphael Chegeni amesema kuwa mfumo wa uthibiti wa mawasiliano uliokabidhiwa kwenye mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) ni uwekezaji tosha.

Ameyasema hayo jijini Dar es salaam mara baada ya kukamilika kwa hafla ya makabidhiano ya mfumo huo, ambapo amesema kuwa huo ni uwekezaji tosha ambapo amesema kuwa serikali inatakiwa kukusanya mapato ya kutosha.

Amesema kuwa kama mfumo huo utasimamiwa vizuri, serikali itakusanya mapato ya kutosha ambayo yataisaidia nchi kupiga hatua za kimaendeleo.

“Kwakweli huu ni uwekezaji mkubwa sana kama serikali itaweka usimamizi mzuri, kwakuwa mimi ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya uwekezaji nitahakikisha nashiriki vizuri katika usimamizi wa uwekezaji,”amesema Dkt. Chegeni

Video: Mhandisi Kilaba aufagilia mfumo wa TTMS
Mwanamke mgonjwa wa macho apewa dawa za nguvu za kiume, zamjeruhi

Comments

comments