Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Oktoba 10, 2016 amekutana na Mwenyekiti wa Kampuni ya Ujenzi ya CRCC ya China, Fengchao Meng ambaye ameahidi kuwekeza kwa kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya mkoa wa Dodoma.

Majaliwa amesema kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni uendelezaji wa Makao Makuu Dodoma, hivyo amezitaja fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda.

Wakati akizungumza na Meng ofisini kwake Magogoni jijini Dar es Salaam, Majaliwa amesema China na Tanzania ni marafiki wa muda mrefu na mataifa hayo yanashirikiana vizuri katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali hivyo Serikali inatarajia mengi kutoka kwenye kampuni hiyo ambayo tayari imeunga mkono juhudi sa Serikali na kuadihi kuwekeza nkatika ujenzi wa miundombinu. Bofya hapa kutazama video

Riyad Mahrez: Leicester City Walinizuia Nisiende Arsenal
Gareth Southgate Amtema Wayne Rooney