Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Magomeni kutumia utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa wakati.

Majaliwa ametoa agizo hilo leo Novemba 18, 2016 wakati alipokagua ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) eneo la Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

Waziri Mkuu amewataka wataalamu hao waendelee kufanya kazi hiyo kwa kufuata misingi ya weledi wa taalauma yao kwani Serikali inawaamini.

“Muhimu mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili wananchi waliokuwa wanaishi hapa waweze kurudi katika makazi yao,” – Majaliwa

Video: Endeleeni kushirikiana na Serikali - Majaliwa
Francesc Arnau: Tulishindwa Kumlipa Mshahara Balotelli