Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kuanzisha kampeni ya kupanda miti katika jiji la Dar es salaam na kuomba zoezi hilo kuwa endelevu na la kuigwa katika mikoa mingine nchi nzima kwani miti ni muhimu na ndiyo inayodhalisha madawa.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati akizindua kampeni ya upandaji miti jijini Dar es salaam mapema leo Oktoba 1, 2016 na kuwaomba  watanzania kuwalea watoto wao katika misingi ya kutunza mazingira, pia alielezea  faida za miti ikiwemo kutengeneza hali ya hewa nzuri kuondoa sumu itokanayo na kemikali mbalmbali ambazo hudhalishwa katika shughuli za kijamii.

Video: RC Makonda atangaza adhabu kwa waharibifu wa mazingira Dar
Simba, Yanga Watoshana Taifa, Kazimoto atema cheche baada ya mechi