Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka Watendaji wote wa Mitaa na Kata kubandika majukumu yao ya kikazi katika mbao za matangazo ya ofisi zao ili kuwawezesha wananchi kutambua na kuweza kuchukua hatua stahiki kama watumishi hao wataenda kinyume na majukumu yao.

Makonda amesema hayo katika Wilaya ya Ilala akiwa katika ziara yake ya wilaya zote za Dar es salaam, ambapo ameeleza kuwa nia na malengo ya ziara hiyo ni kupima uwajibikaji wa watumishi na kuona kama wananchi wanaridhika na utendaji kazi wa watumishi katika mkoa huo.

Real Madrid Kumuharakisha Gareth Bale
Video: Tatizo nikimpigia simu Maalim Seif hapokei - Prof. Lipumba