Siku moja baada ya kusambaa kwa video inayomuonesha Justin Bieber akipigana na shabiki mkubwa kumzidi, rafiki yake wa karibu, bondia Mayweather amemsifia kwa tukio hilo.

Ingawa Mayweather ameeleza kuwa hafahamu chanzo cha ugomvi kati ya Bieber na jamaa huyo, amesema kuwa ameonesha kuwa yeye sio ‘boya’ na amempa heshima.

“Watu wanaweza kusema wanachosema, lakini mwisho wa siku Justin Bieber ameonesha kuwa ana moyo na ameonesha yeye sio ‘boya’. Yote kwa yote ni heshima,” alisema.

Bieber alionekana akikunjana na kupigana na jamaa ana mwili mkubwa, usiku wa Jumatano huko Cleveland, Marekani.

Suarez Apandisha Mzuka, Uruguay Ikitolewa Copa America
Video: Obama amuidhinisha Hillary Clinton Urais wa Marekani