Mgombea wa kiti cha Urais wa Shirikisho la Madereva Tanzania (TDF), Wito Zabron Mbwilo amejiuzulu nafasi hiyo dakika chache kabla ya kupigwa kura.

Wito alijiuzulu kugombea nafasi hiyo na kumfanya mgombea mwenza Abdallah Libula kupita bila kupingwa.

Uchaguzi huo ulifanyika jana jijini Dar es salaam mara baada ya wananchama wa vyama vya Madereva kutoka mikoa yote nchini kukutana kwa ajili ya kuunda shirikisho hilo, kujadili na kupitisha Katiba na kuchagua viongozi wa shirikisho hilo.

“Nimeamua kujiuzulu nafasi hii, kwasababu binafsi nimemkubali sana mgombea mwenzangu ninayeshindana naye kwakuwa anafanya vizuri, hivyo kura yangu nampigia yeye,” amesema Mbwilo

Aidha, Mbwilo ambaye ni mwenyekiti wa waendesha Bodaboda jijini Mbeya amesema kuwa katika mkoa anaotoka kuna changamoto kubwa ambazo anaamini kupitia shirikisho hilo zitapata utatuzi na sasa yatakuwepo maendeleo kwa madereva.

Hata hivyo, Mbwilo amewataka waendesha bodaboda wa jiji la Mbeya kutii sheria bila shuruti kwani kutapunguza ajali mbalimbali zisizo na ulazima.

Polisi wakanusha taarifa za kushambuliwa gari la Mbunge
Chadema: Mawakala wetu wananyanyaswa kwenye vituo vya kupigia kura

Comments

comments