Mlezi wa msanii aliyefariki dunia maarufu kwa jina la ‘Dogo Mfaume’ ameelezea ugonjwa uliokuwa unamsumbua msanii huyo mpaka kumsababishia kifo ambapo amesema kuwa kilichokuwa kinasubiriwa ni kufanyiwa operesheni tu.

Amesema kuwa Dogo Mfaume alianza kupoteza sauti taratibu baadaye sauti ilikata na kushindwa kuongea hali iliyopelekea kumpelekea hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuchukua vipimo ambapo iligundulika kuwa alikuwa na uvimbe ndani ya kichwa.

Hayo yamesemwa na Pili Misana alipokuwa akizungumza na Dar24, amesema kuwa wakati akiandaliwa kufanyiwa opresheni siku moja kabla ya Operesheni hali yake ilibadilika ghafla na ndipo umauti ulipomkuta.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 19, 2017
Serengeti Boys Yaichapa Angola, Kombe la Dunia Lileee....!