Jukwaa huru la wazalendo Tanzania limempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kwa kuteua asilimia 70% ya wakuu wa wilaya vijana na kusema kuwa wana muunga mkono katika uongozi wake.

Hayo yamesemwa na Katibu mkuu wa jukwaa hilo Bw,Mtela Mwampamba alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake. ’’Jukwaa limefurahishwa na Mh. Magufuli kwa kuzidi kujipambanua zaidi kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wote pasipo kujali itikadi zao hususani za vyama vya kisiasa’’-Mwampamba’’

Mbeya City Waachana Na Haningtony Kalyesubula
Video: Makonda akitangaza kumsimamisha kazi 'Engineer' mkuu wa mkoa wa Dar